Mshambuliaji wa Simba Adam Salamba ambaye jana aliumia kwenye mchezo wa robo fainali ya kombe la Kagame dhidi ya AS Ports, ameweza kufanya mazoezi ya jioni na kikosi Simba leo.
Salamba alipata majeraha ya nyama za paja jana lakini habari njema ni kwamba mshambuliaji huyo huenda akawa fiti kucheza mchezo wa nusu fainali.
Simba imeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo wa nusu fainali ambapo mpinzani wake atafahamika baada ya kukamilika kwa michezo miwili ya robo fainali leo.
Wakati huo huo Azam FC imetinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Kagame baada ya kuilaza Rayon Sports mabao 4-2.
Mabao yote ya Azam FC yalifungwa na Shabani Iddi ambaye sasa anaongoza kwenye orodha ya wafungaji bora wa michuano hiyo akiwa na mabao saba.

ADVERTISE HERE