Uongozi wa klabu ya Gor Mahia uko tayari kumuuza kiungo wake tegemeo Francis Kahata kwa klabu ya Simba lakini sio sasa.
Gor Mahia inayoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho ikiwa kundi moja na Yanga, Rayon Sports na USM Alger, imedai wakati huu inamuhitaji Kahata ili kuweza kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.
Lakini wamedai wako tayari kumuachia mchezaji huyo mwezi wa 12.
Kahata amekuwa katika kiwango bora kilichowavutia viongozi wa Simba ambao tayari wamemsajili Meddie Kagere aliyemaliza mkataba kwenye klabu ya Gor Mahia.
"Juhudi zetu na kumsajili KaÂhata bado tunaendelea nazo lakini Gor Mahia wamekuwa wagumu sana kumwachia na wametuambia kuwa bado waÂnahitaji huduma yake katika michuano ya kimataifa.
"Wametuambia kuwa kama tunamtaka kweli basi wao watamwachia mwezi Desemba mwaka huu, lakini kwa sasa itakuwa ni ngumu," gazeti la Championi limemnukuu mmoja wa viongozi wa Simba.

ADVERTISE HERE