Djuma asifu kiwango cha Wawa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Jul 2018
Djuma asifu kiwango cha Wawa
Kwenye michezo yake mitatu ya kwanza katika michuano ya kombe la Kagame, beki mpya wa Simba Paschal Serge Wawa hakuonyesha kiwango cha kuridhisha kupelekea kuibua hofu miongoni mwa mashabiki wa mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Lakini kwenye mchezo wa jana wa robo fainali dhidi ya AS Ports, Wawa alionyesha kiwango cha hali ya juu.

Akizungumza baada ya mchezo huo ambao Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kufanikiwa kufanikiwa kutinga nusu fainali, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Masudi Djuma amewataka mashabiki kuwa watulivu, waache kuingilia kazi ya benchi la ufundi.

Djuma amemsifia Wawa kuwa ni mchezaji mzuri na ameridhihirisha hilo jana.

"Si niliwaambia muache mambo ya kuita wachezaji wazee?, mzee gani anakimbia dakika 90 uwanjani?. Wawa si mzee bali ni MZEE WA KAZI, lazima uwe na wazee wa kazi ili waungane na vijana kama akina Mlipili wanaochipukia," amesema Djuma

"Wawa ni experienced, anatumia akili nyingi, mnadhani kwa kiwango alichoonyesha leo nikiwauliza TUMFUKUZE au TUSIMFUKUZE, mtajibu nini?"
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
13h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
16h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’