Brazil imeondoshwa kwenye michuano ya kombe la Dunia baada ya kulazwa mabao 2-1 na Ubelgiji kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa Ijumaa usiku.
Licha ya Brazil kutawala mchezo kwa muda mwingi, ni Ubelgiji iliyokuwa hatari kupitia mashambulizi yake ya kushitukiza.
Mabao yote ya Ubelgiji yalipatikana kwenye kipindi cha kwanza wafungaji wakiwa Fernadinho (OG) na Kelvin De Bruyne.
Bao pekee la Brazil lilipatikana kwenye dakika ya 76 likifungwa na Renato Augusto.
Matokeo hayo yameipeleka Ubelgiji nusu fainali ambapo sasa itachuana na Ufaransa katika hatua hiyo.
Mapema kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali Ufaransa ilikata tiketi ya kutinga nusu fainali baada ya kuichapa Uruguay kwa mabao 2-0.

ADVERTISE HERE