Mashabiki wa Simba kwa sasa kiroho safi baada ya kupatikana kwa muarobaini wa mabao pale nyota wao; John Bocco na Emmanuel Okwi wanapokosekana uwanjani kufuatia moto walioanza nao mastraika wapya, Meddie Kagere na Adam Salamba.
Wawili hao walioifungia Simba mabao matano mpaka sasa kwenye michuano ya Kombe la Kagame, wamekuwa wakionyesha ushirikiano mzuri unaoibeba timu yao na Salamba ameeleza huu ni mwanzo nzuri kwao kama wataendelea kushirikiana.

Straika huyo aliyetua Simba akitokea Lipuli, alisema katika mechi aliyocheza dhidi ya APR ya Rwanda akiwa sambamba na Kagere alijiona mchezaji wa tofauti baada ya staa huyo aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia ya Kenya kumwelekeza namna ya kufunga.
“Nimeamini mzoefu ni mzoefu tu, kucheza mechi moja na Kagere amenifunza mengi, kwanza namna ya kumpasia mipira ya kufunga, jinsi alivyokuwa ananipa pasi na kunielekeza cha kufanya nikiwa nimebanwa na mabeki,†alisema.
Mbali na ufundi alioanza kuupata kwa Kagere, pia aliweka wazi mambo matatu aliyoyaona ndani ya kikosi hicho kwamba amebaini bila kufunga, kuwa na umakini na kujituma basi anaweza akajikuta anakuwa na maisha magumu mbele ya mastraika wakongwe.
“Kabla ya kujiunga na Simba nilikuwa nasikia klabu kongwe zina presha na kila mechi zinahitaji ushindi, jambo hilo kwa sasa nimeanza kuonja joto lake, lakini inanifundisha kutojisahau kwa kilichonileta, naamini nitafanya kitu cha tofauti,†aliongeza.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE