Yanayojiri Urusi : Robo fainali France vs Uruguay, Brazil vs Belgium

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Jul 2018
Yanayojiri Urusi : Robo fainali France vs Uruguay, Brazil vs Belgium
Baada ya mapumziko ya siku mbili, michuano ya kombe la dunia hatua ya robo fainali inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa huko Urusi.

Mchezo wa mapema saa 11 jioni ni kati ya Uruguay dhidi ya Ufaransa na kufuatiwa na mchezo wa pili kati ya Brazil dhidi ya Ubelgiji.

Ufaransa inapewa nafasi kubbwa ya kuibuka na ushindi dhidi ya timu isiyofungika kwa urahisi, Uruguay ambayo itamkosa kinara wake wa mabao Edison Cavan.

Hata hivyo takwimu zinaibeba zaidi Uruguay kwani haijawahi kufungwa na Ufaransa kwenye michuano ya kombe la dunia lakini pia Ufaransa imeshinda mara moja tu katika michezo saba ambayo timu hizo zimekutana.

Hata hivyo kikosi cha Ufaransa wakati huu kinaingia kwenye mchezo huo kikiwa na 'moto' kutokana na ukali wa safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na kinda mwenye kasi ya umeme Kylian Mbappe.

Mchezo wa pili kati ya Brazil dhidi ya Ubelgiji unatajwa kama mchezo wa fainali kabla ya fainali.

Timu zote zimesheheni wachezaji wenye vipaji na wengi wametabiri timu itakayoibuka na ushindi kwenye mchezo huo itakuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa.

Wakati Brazil ikiwategemea zaidi washambuliaji wake Neymar, Gabriel Jesus na Coutinho, Ubelgiji itabebwa na Eden Hazard, Lukaku na De Bruyne.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’