Kuna uwezekano mkubwa kwa timu zote za Tanzania kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Kagame inayoendelea jijini Dar es salaam.
Vilabu vya Simba, Singida United na Azam FC tayari vimejihakikishia kutinga robo fainali huku JKU yenye alama nne ikiwa na matarajio makubwa ya kufuzu kupitia 'best looser'.
Jana Azam FC ilimaliza kileleni mwa kundi A baada ya kuilaza JKU mabao 2-1 na kufikisha alama saba huku Vipers ya Uganda nayo ikitinga robo fainali baada ya kuilaza Kator mabao 3-0 na kufikisha alama sita.
Hatua ya makundi inatarajiwa kukamilika leo saa 12 jioni kwa michezo miwili ya kundi B kupigwa ambapo Gor Mahia itacheza na AS Ports uwanja wa Taifa wakati kule uwanja wa Azam Complex, Chamazi Lydia itacheza na Rayon Sports

ADVERTISE HERE