Wasifu wa kocha mpya anayetua Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
5 Jul 2018
Wasifu wa kocha mpya anayetua Simba
Patrick Winand Aussems alizaliwa, Februari 6, 1965 katika mji wa Moelingen, Ubelgiji na kuicheze RCS Vise kati ya 1974-81, klabu iliyokuja kufilisika mwaka 2014.

Patrick alikipiga pia Standard Liege (1981-88), kisha kutua K.A.A Gent (1988-19), R.F.C Seraing (1989-90) na ES Troyes AC (1990-93).

Baada ya kustaafu mwaka 1993 kama Kocha Mchezaji wa Troyes inayoshikili Ligue1, alijitosa jumla kuwa kocha ndani ya klabu hiyo hadi 1995 alipotua Saint Lousienne ya Re Union.

Klabu nyingine alizofundisha ni Capricorne Saint-Pierre, Stade Beaucairois, Stade de Reims, KSA Cameroon, SCO Angers, Evian Thonon Gaillard F.C, Shenzhen Ruby, Chengdu Blades na kutua kwa waliokuwa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika 2012 AC Léopards akimpokea Joseph Omog aliyekuwa ameletwa nchini kuinoa Azam FC.

Alianza kuinoa timu hiyo tangu mwaka 2013-15 ambapo chini yake aliisaidia Leopards kubeba taji la Ligi Kuu ya Congo msimu wa 2014 bila upoteza mechi na iliruhusu kufungwa bao moja tu na kuifikisha timu hiyo katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho ikipoteza mbele ya Sewe Sports ya Ivory Coast hiyo ikiwa imeng’oka Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huo.

Alipotoka AC Leopard alichukuliwa El Hilal ya Sudan kabla ya kutemwa miezi michache baada ya timu kupata matokeo mabaya na kutua timu ya taifa ya Nepal aliyoinoa kati ya 2015-16.

Anasifika kwa soka la kushambulia sambamba na kujilinda na kama atamalizana na mabosi wa Simba iliyo chini ya Bilionea, Mohammed ‘Mo’ Dewji ni wazi Wekundu wa Msimbazi watakimbiza sana, kwani Patrick ni bonge la kocha.

Kwa hisani ya Mwananspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →