Beki Paschal Serge Wawa tayari amesajiliwa na Simba kuchukua nafasi ya Mganda Juuko Murshid anayeelezwa kutimkia Afrika Kusini.
Wawa alitambulishwa na uongozi wa Simba sambamba na Meddie Kagere na Deogratius Munishi siku moja kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame.
Hata hivyo beki huyo ameonekana kuwa mzito katika michezo aliyocheza ya kombe la Kagame.
Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Masudi Djuma anahitaji kuufanyia kazi mwili mkubwa wa Wawa ili awe mwepesi kuweza kukabiliana na washambuliaji wenye kasi.
Katika michezo aliyocheza kwenye Kagame Cup, ameshindwa mara kadhaa kwendana na kasi ya washambuliaji wa timu pinzani.
Ukiondoa mapungufu hayo, Wawa ameonyesha uwezo mkubwa wa kupiga pasi na kuweza kuanzisha mashambulizi kutokea nyuma.

ADVERTISE HERE