Simba na Singida United zatoshana nguvu kombe la Kagame

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Jul 2018
Simba na Singida United zatoshana nguvu kombe la Kagame
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Singida United kwenye mchezo kumaliza hatua ya makundi, michuano ya kombe la Kagame.

Simba ilitangulia kupata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wake mpya Meddie Kagere akifunga bao lake la pili kwenye michuano hiyo.

Kagere aliutumbukiza mpira kimiani kwa kichwa akiunganisha krosi ya Jamal Mwambeleko

Hata hivyo makosa ya Mzamiru Yassin yalimpa nafasi Danny Lyanga kuirejesha Singida United mchezoni kwenye dakika ya 35 kwa kufungia bao safi la kusawazisha.

Kwa ujumla kikosi cha Simba kimecheza vizuri mchezo huo ukiondoa makosa madogo madogo yaliyokuwa yakifanywa kwenye safu ya ulinzi.

Singida United nayo ilitoa upinzani mkali kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Kocha Masudi Djuma anatumia michuano hii kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji ambao hawakutumika sana msimu uliopita.

Matokeo hayo yanaifanya Simba imalize kinara wa kundi C baada ya kufikisha alama saba sawa na Singida United lakini Simba imefunga mabao mengi zaidi.

Katika mchezo mwingine uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi, APR imeifumua Dakadaha kwa mabao 4-1.

Simba na Singida United zimetinga robo fainali huku APR ikiwania moja ya nafasi mbili za 'best looser' sambamba na timu nyingine za kundi B na A ambazo zitashindwa kumaliza katika nafasi za kufuzu moja kwa moja
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
17h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
17h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
20h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’