Simba yaomboleza kifo cha Prof Maji Marefu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Jul 2018
Simba yaomboleza kifo cha Prof Maji Marefu
TAARIFA KWA UMMA

Klabu ya Simba imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mmoja wa Wanachama wake mwandamizi Mh. Stephen Ngonyani uliotokea jana hapa jijini kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mh Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu atakumbukwa sana na Wanasimba kwa mchango wake mkubwa katika masuala mbalimbali yaliyoiwezesha klabu yetu kufika hapa ilipo.

Hivyo kaimu Rais wa klabu Bwana Salum Abdallah Muhene, viongozi wote, wanachama, wachezaji na washabiki wote wanatoa pole kwa Spika wa Bunge na Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuondokewa na Mbunge mwenzao ambae alikuwa akiwakilisha wananchi wa Jimbo la Korogwe vijijini.

Pia tunatoa pole kwa Wananchi wote wa jimbo hilo ambalo Mh Ngonyani alilitumilkia kwa uadilifu mkubwa.

Sanjari na hayo klabu inawapa pole sana familia na wafiwa wote na inawaomba wawe na subira kwenye kipindi hiki kigumu kwao.

IMETOLEWA NA HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI SIMBA SPORTS CLUB
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
29m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’