Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba saa kumi jioni watashuka kwenye uwanja wa Taifa kucheza na Singida United katika mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Kagame inayoendelea jijini Dar es salaam.
Mchezo huo wa kundi C ni wa kukamilisha ratiba tu kwani tayari timu zote zimeshatinga robo fainali ya michuano hiyo.
Simba itaongozwa na mshambuliaji wake mpya Meddie Kagere aliyesajiliwa kutoka klabu ya Gor Mahia wiki iliyopita.
Kagere alianza kuitumikia Simba juzi kwenye mchezo dhidi ya APR na kuisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 yeye akifunga bao la ushindi kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 89.
Mshambuliaji huyo atashirikiana na Adam Salamba ambaye ndiye kinara wa mabao kwenye michuano hiyo akiwa ameifungia Simba mabao matatu.
Ratiba ya Michezo ya yote leo

ADVERTISE HERE