Mwaka 2003, Mtibwa Sugar ilifungiwa na CAF kutoshiriki michuano yoyote inayosimamiwa na shirikisho hilo kutokana na kushindwa kwenda kucheza dhidi ya Santos FC ya Afrika Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Mtibwa ilishindwa kwenda Afrika Kusini kutokana na kile kilichodaiwa kuwa uongozi wa klabu hiyo ulikosa fedha za nauli za kuisafirisha timu hiyo kwenda nchini humo.
Baada ya kutwaa taji la FA (ASFC) msimu uliomalizika, Mtibwa Sugar imefuzu kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje kwa miaka 15.
Shirikisho la soka nchini (TFF) lilituma jina la Mtibwa Sugar CAF ili kupata maelekezo juu ya hatma ya adhabu ya klabu hiyo.
Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amewaambia waandishi wa habari leo kuwa Mtibwa Sugar itaruhusiwa kushiriki michuano kombe la Shirikisho kama itaweza kuilipa gharama za klabu ya Santos kabla ya Julai 20 2018.
Pia Mtibwa Sugar inatakiwa ilipe faini ya dola 1500 (Mil 3.5) kabla ya tarehe hiyo iliyotajwa hapo juu.

ADVERTISE HERE