Yanayojiri Urusi : Uingereza yatinga robo fainali, itacheza na Sweden

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Jul 2018
Yanayojiri Urusi : Uingereza yatinga robo fainali, itacheza na Sweden
Uingereza imefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la dunia kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Colombia.

Uingereza ilitangulia kufunga kwenye mchezo huo katika dakika ya 57 kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Harry Kane baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari na Carlos Sanchez.

Hata hivyo wakati mchezo huo ukielekea ukingoni, beki Yerri Mina aliisawazishia timu yake katika dakika ya 93 hilo likiwa ni bao lake la tatu katika mashindano hayo hivyo kuupeleka mchezo huo kwenye dakika 30 za nyongeza na baadae mikwaju ya penati.

Harry Kane, Rashford, Trippier na Dier walifunga mikwaju yao ya penati huku Jordan Henderson akikosa.

Colombia walikosa mikwaju miwili.

Uingereza sasa itachuana na Sweden kwenye mchezo wa robo fainali.

Mapema Sweden ilitinga robo fainali baada ya kuilaza Uswisi kwa bao 1-0.

Mchezo huo umekamilisha hatua ya 16 bora ambapo Uruguay, Ufaransa, Urusi, Ubelgiji, Brazil, Sweden, Uingereza na Croatia zimetinga robo fainali.

Michezo ya robo fainali itapigwa Ijumaa na Jumamosi ambapo siku ya Ijumaa, 06 July, Uruguay itacheza na Ufaransa saa 11 jioni huku mchezo unaofuata ukiwa kati ya Brazil dhidi ya Ubelgiji saa tatu usiku.

Jumamosi, July 07, Uingereza itacheza na Sweden saa 11 jioni wakati Urusi itaikabili Croatia saa tatu usiku.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
44m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’