Yanayojiri Urusi : Brazil, Ubelgiji zatinga robo fainali kombe la Dunia

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Jul 2018
Yanayojiri Urusi : Brazil, Ubelgiji zatinga robo fainali kombe la Dunia
Brazil na Ubelgiji zimefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo yao ya hatua ya 16 bora iliyopigwa Jumatatu, Julai 02, 201.

Wakati Ubelgiji ikipata ushindi wa tabu wa mabao 3-2 dhidi ya Japan, Brazil ilifanikiwa kuilaza Mexico mabao 2-0.

Mabao ya Brazil yote yalipatikana katika kipindi cha pili yakiwekwa kimiani na washambuliaji Neymar Da Silva na Firmino aliyefunga wakati mchezo huo ukielekea ukingoni akimalizia kazi nzuri ya Neymar.

Winga wa Chelsea Willian anayewindwa na klabu ya FC Barcelona ndiye aliyetengeneza bao la kwanza la Brazil lililofungwa na Neymar.

Brazil iliuanza mchezo huo taratibu na Mexico kufanikiwa kutawala kwenye kipindi cha kwanza huku ikifanya mashambulizi ya kushitukiza.

Hata hivyo hali ilikuwa tofauti kwenye kipindi cha pili kwa Brazil kulishambulia lango la Mexico kwa muda mwingi na kufanikiwa kufunga mabao hayo yaliyowapeleka robo fainali.

Mexico imeendeleza rekodi mbovu ya kuishia hatua ya 16 bora sasa ikiwa imeondolewa katika hatua hiyo kwa mara ya saba mfululizo.

Ubelgiji ililazimika kutoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda 3-2 katika mchezo ambao Japan ilitoa upinzani mkali.

Japan ilihitaji dakika nne tu kufunga mabao yake mawili mapema tu kwenye kipindi cha pili kupitia kwa Haraguchi ma Inui.

Lakini wachezaji wa Ubelgiji wakiongozwa na nyota wao Eden Hazard, Kelvin De Bruyne na Romelu Lukaku hawakukata tamaa na juhudi zao zilizaa matunda kwa kupachika mabao yao kupitia kwa Vertonghen, Fellain na Chadli aliyefunga bao la ushindi kwenye dakika za nyongeza.

Brazil na Ubelgiji sasa zitachuana kwenye mchezo wa robo fainali
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’