Mabao ya Adam Salamba na Meddie Kagere yameiwezesha Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya APR kwenye mchezo wa kombe la Kagema uliopigwa katika dimba la Taifa Jumatatu jioni.
Kagere aliyesajiliwa na Simba akitokea klabu ya Gor Mahia alifunga bao lake la kwanza akiwa katika uzi wa Wana Msimbazi kupitia mkwaju wa penati kwenye dakika ya 89.

Ushindi huo umeipeleka Simba robo fainali ya michuano hiyo baada ya kufikisha alama sita ikishinda michezo yake miwili.
Adam Salamba ameendelea kung'ara kwenye kikosi cha Simba baada ya kufikisha mabao matatu kwenye michuano hiyo.

Mapema Singida United nayo ilitinga robo fainali baada ya kuilaza Dakadaha ya Somalia kwa bao 1-0.
Simba na Singida United zimejihakikishia kutinga robo fainali baada ya kushinda michezo yao yote miwili.
Zitachuana kwenye mchezo wa kukamilisha ratiba keshokutwa, Julai 04 2018.

ADVERTISE HERE