Wawa aahidi kuipa Simba ubingwa kombe la Kagame

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Jul 2018
Wawa aahidi kuipa Simba ubingwa kombe la Kagame
Beki Paschal Serge Wawa aliyesajiliwa na Simba hivi karibuni ameahidi kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa kombe la Kagame.

Beki huyo raia wa Ivory Coast amesema atatumia uzoefu wake wa michuano ya Kimataifa kuisaidia Simba ing'are kwenye michuano hiyo inayofanyika jijini Dar es salaam.

"Kikubwa nitahakikisha natoa uzoefu wangu wote kwa wenzangu kuhakikisha wote tunafikia malengo katika haya mashindano kwa sababu najua ugumu na ushindani wake ulivyo," amesema Wawa

"Ukiangalia bado tunacheza na wachezaji ambao ni wageni kwangu sasa lazima nifanye kitu kama hicho ili watu waone tofauti na siyo kuangalia umri wangu," Wawa ameliambia gazeti la Sports Xtra.

Wawa ametua Simba akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia klabu ya El Marreikh ya Sudani.

Amesajiliwa Simba kuchukua nafasi ya Juuko Murshid anayesemekana kuwa mbioni kutimkia Afrika Kusini katika klabu ya SuperSport United.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’