Salamba na Kaheza walivyoiangamiza Dakadaha

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Jul 2018
Salamba na Kaheza walivyoiangamiza Dakadaha
Safu mpya ya ushambuliaji ya Simba, imetoa taswira ya upana wa kikosi kitakavyokuwa kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba ambao wamelenga kuongeza upana wa wigo wao wa safu ya ushambuliaji iliwasajili Adam Salamba (Lipuli) , Marcel Kaheza (Majimaji) na Mohammed Rashid (Tanzania Prisons) ili kukidhi mahitaji hayo.

Washambuliaji hao, walianza kukitumikia kikosi hicho kwenye michuano ya Sportpesa nchini Kenya, lakini walionekana kushindwa kuonyesha ubora wao.

Kaheza na Salamba wameonekana kuanza kuelewana kwenye mchezo wa kwanza wa kombe la Kagame kwa kuifunga mabao muhimu timu hiyo kwenye mchezo wa kwanza wa Simba dhidi ya Dakadaha.



Katika mchezo huo uliochezwa jana Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Wasomalia hao.

Kaheza ambaye alitumika kwenye mchezo huo kama winga wa aliyekuwa anatokea pembeni ndiye aliyekuwa wa kwanza kuifungia Simba bao la kwanza kwa njia ya mkwaju wa penalti dakika ya tisa ya mchezo.

Bao la pili kwa Simba lilifungwa na Adam Salamba kwa shuti baada ya kuchongwa krosi na beki wa kulia, Shomary Ally.

Kabla ya mapumziko Simba ilijipatia bao la tatu kupitia kwa Rashid Juma ambaye alikuwa akicheza winga ya upande wa kushoto.

Salamba na Kaheza ambao walianza kwenye eneo la ushambuliaji kwenye kipindi hicho cha kwanza japo mmoja alikuwa akitokea pembeni walionekana kuwa na maelewano mazuri.

Mara kadhaa Salamba alitumia ukubwa wa mwili wake kushuka chini na kusaidia kukaba pindi walipokuwa wanapoteza mipira huku nafasi yake juu ikizibwa vizuri na Moses Kitandu aliyekuwa akicheza namba 10.

Upande wake Kaheza naye alikuwa akisogea kwenye eneo la kiungo na kumuongezea nguvu, Mzamiru Yassin.

Wakati Salamba na Kaheza wakicheza vizuri kipindi hicho cha kwanza, Pascal Wawa ambaye naye ni usajili mpya kwenye kipindi hiki cha usajili alionyesha kiwango cha juu kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Kipindi cha pili, Simba iliendelea kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa huku wakionekana kuwa na uhai zaidi kwenye eneo la kiungo ambalo alikuwa akicheza Mzamiru na mkongwe Mwinyi Kazimoto.



Salamba aliipatia bao la nne Simba kwa kuachia shutu kali nje ya kumi na nane lililomshinda mlinda lango wa Dakadaha, Mustaf Hussein.

Simba ilifanya mabadiliko kadhaa kwenye kipindi hicho cha pili kwa kuwatoa, Kaheza, Kitandu, Rashid huku nafasi zao zikichukuliwa na Mohammed Rashid, Said Ndemla na Abdul Hamis.

Mabadiliko hayo yaliiendelea kuifanya Simba kumiliki mpira kwa asilimia kubwa huku ikilisakama lango la Dakadaha hadi mwisho wa mchezo.

"Tulicheza vizuri japo kuna makosa madogo ambayo yalikuwa ya kifanyika, nimefurahishwa na namna ambavyo washambuliaji wangu wamecheza, bado tuna muda wa kuendelea kuwa pamoja kwa hiyo kunauwezekano wa kuendelea kuona vitu vizuri kutoka kwao," alisema Masoud Djuma

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’