Simba kuwakabili Wasomali kombe la Kagame leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Jun 2018
Simba kuwakabili Wasomali kombe la Kagame leo
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wanatarajia kuanza kampeni ya kuwania taji la Kombe la Kagame kwa kuwakaribisha Dakadaha kutoka Somalia katika mechi ya Kundi C itakayofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kwenye mchezo huo Simba itawakosa nyota wake muhimu kama nahodha, John Bocco, Emmanuel Okwi, Erasto Nyoni, Aishi Manula, Shomari Kapombe na Asante Kwasi.

Hata hivyo Kaimu Kocha Mkuu wa SImba, Masoud Djuma, amesema kuwa anakiamini kikosi chake kitakachopambana kuwania ubingwa wa michuano hiyo na kuongeza hii ni nafasi nzuri kwa wachezaji watakaoshiriki kuonyesha uwezo wao.

Djuma amesema Simba haijadharau michuano hiyo na hali ya nyota hao kuwa majeruhi ndiyo imewafanya wawaondoe kwenye michuano hiyo inayofanyika kwa kushirikisha timu 12 kutoka katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Kocha huyo alisema kuwa wanatarajia kutumia wachezaji wenye uwezo lakini hawakupata nafasi nzuri kwenye ligi na nyota wapya waliosajiliwa ili kuwapa nafasi ya kuonyesha viwango vyao ili msimu ujao utakavyoanza waweze kuisaidia timu kutetea ubingwa waliouchukua hivi karibuni.

"Tutashinda kombe hilo bila ya kuwapo fulani na fulani, hatujaidharau michuano hii, ila wale tumewaambia wapumzike kwa sababu ni wagonjwa, mechi nyingi walicheza wakiwa wagonjwa, baada ya Kagame kuna ligi na katikati kuna Ligi ya Mabingwa Afrika," alisema Djuma.

Aliongeza kuwa kila mechi kwao ni sawa na fainali na hawataidharau timu yoyote watakayokutana nayo kwenye michuano hiyo.

"Tumefanya mazoezi vizuri na kila mara nimekuwa nikiwaambia wachezaji wangu wanatakiwa kujituma na kuonyesha uwezo wao, chini yangu kila mmoja atapata nafasi ya kucheza, tunataka kufikia hatua ukitoa kitu, unaingiza kitu," aliongeza kocha huyo raia wa Burundi.

Baada ya mechi hiyo ya Simba itakayofanyika kuanzia saa 8:00 mchana kumalizika, AS Ports ya Djibout itachuana na Lydia Ludic kutoka Burundi.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’