Kwa muda wa wiki mbili klabu 12 kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) zitasaka ubingwa wa Kombe la Kagame 2018.
Michuano hiyo ya 41 tangu kuasisiwa kwake mwaka 1974, itachezwa kuanzia leo Ijumaa mpaka Julai 13 atakapofahamika bingwa wa mwaka huu, huku timu za Tanzania Bara wakiwamo watetezi Azam, Mabingwa wa Kihistoria, Simba na Singida United zikiwa na kibarua kizito na wenzao wa JKU kulibakisha taji hilo nyumbani.
Timu nyingine shiriki ni APR na Rayon Sports za Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya Burundi, Dakadaha ya Somalia, Viper ya Uganda na Kator ya Sudan Kusini.
Pazia la michuano hiyo linafunguliwa kwa mchezo kati Vipers na JKU kabla ya watetezi Azam FC kuliamsha dhidi ya Kator ya Sudan Kusini kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ilihali Singida United na APR zitamalizana Uwanja wa Taifa.
Kuelekea kwenye michuano hiyo, kila shabiki ana mtazamo wake juu fainali hizo za 41, lakini Mwanaspoti linaiangazia Simba ambao ndio mabingwa wa kihistoria wakilibeba taji hilo mara sita ikiwa ni nyingine kuliko timu yoyote zilizowahi kushiriki.
Mabingwa hao wa Tanzania ambao kesho Jumamosi wataliamsha dhidi ya Dakadaha, wamekuwa kambini tangu warejee kutoka kwenye fainali za SportPesa Super Cup walipoambulia nafasi ya pili baada ya kuzidiwa ujanja na Gor Mahia ya Kenya.
Simba inaingia katika michuano hiyo ikiwa imeongeza nguvu katika kikosi chake, japo itawakosa nyota wake wengi wa kikosi cha kwanza waliopo mapumzikoni, ila kwa maandalizi iliyofanya kuna kila dalili wababe hao kulinyakua taji hilo tena.
REKODI
Mara ya mwisho kwa Simba kubeba taji hilo ilikuwa mwaka 2002 kule Zanzibar ikiwa ni takribani miaka 16 imekihaha kulirejesha na hii ni zamu yao kufanya kweli kulingana na maandalizi iliyofanya chini ya Kocha Masoud Djuma.
Taji la kwanza kwa Simba ilikuwa mwaka 1974, kisha ikakaa muda mrefu kabla ya 1991 ikabeba tena na kulitetea mwaka uliofuata na kusubiri tena hadi 1995 na 1996 ilipobeba mfululizo tena, ndipo ikamalizia mwaka 2002 wakati Rais wa Rwanda, Paul Kagame alipojitosa kuyadhamini mashindano hayo na kufahamika kama Kagame Cup.
Kutokana na kiu waliyonayo mashabiki wa Simba ni wazi huu ni msimu wao, labda tu wachemsha wenyewe nyumbani ikizingatiwa watani wao, Yanga hawapo michuanoni.
KIKOSI KILIVYO
Simba imewapumzisha nyota wake wa kikosi cha kwanza kasoro nahodha, John Bocco ambaye jina lake lipo kwenye orodha ya watakaoshiriki michuano hiyo, hata hivyo, Bocco huenda akajiunga na kikosi hicho baada ya mechi ya kwanza ya kesho.
Wachezaji wote wa kikosi cha kwanza hawatashiriki michuano hiyo wakiandaliwa kurejea wakati wa maandalizi ya Ligi Kuu itakayoanza Agosti.
Simba imekuwa na nyota wenye uwezo wa kuliamsha dude kisawasawa akiwamo kipa Said Mohammed ‘Nduda’ na chipukizi Ally Salim na Deogratius Munishi ‘Dida’ aliyesajiliwa juzi.
Beki wa kulia imeachwa mikononi mwa Ally Shomary akifukia mashimo ya Shomary Kapombe na Nicholas Gyan, huku kushoto atakuwa nahodha msaidizi Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ atakayesaidiana na Jamal Mwambeleko.
Beki ya kati itawahusu zaidi Paul Bukaba akishirikiana na ingizo jipya, Pascal Wawa watakaochukua nafasi za Yusuf Mlipili, James Kotei na Erasto Nyoni.
Kiungo mzoefu Jonas Mkude yupo mapumziko na hivyo kumuachia nafasi Muzamiru Yassin, huku winga wa kulia atasimama chipukizi Rashid Juma na namba nane itaenda kwa Said Ndemla, japo Mwinyi Kazimoto naye anaweza kuliamsha kesho Jumamosi.
Straika wamepewa Adam Salamba na Mohammed Rashid ambao kama watashindwa kufanya vizuri anaweza kuingia Moses Kitandu.
Winga wa kushoto baada ya kutokuwepo kwa Shiza Kichuya atacheza Marcel Kaheza au Mohammed Ibrahim ‘MO’ kuanza kabisa kwani walikuwa wakicheza kwa kupishana mazoezini.
Kocha wa Simba, Masoud Djuma alisema ameiandaa timu yake ili kufanya vizuri ikizingatiwa, Simba ina rekodi tamu ya Kagame tangu mwaka 1974 ikinyakua mara sita ikiwa ndiye kinara mpaka sasa.
“Michuano hiyo itawapa nafasi wachezaji wasiopata namba kwenye ligi mara kwa mara na atakayeonyesha kiwango cha juu anaweza kupata nafasi msimu ujao au kuongezwa mkataba endapo mkataba wake utakuwa umemalizika.
“Tunajua tunakutana na baadhi ya timu ambazo tulikutana nazo katika Mashindano ya Sport Pesa lakini hapa tunacheza nyumbani tuna kila sababu ya kucheza kwa nguvu na kupata matokeo ya ushindi,†alisema Djuma.
Kikosi cha Simba huenda kisitishe sana kama ilivyokuwa kwenye Ligi Kuu kwa kuwapumzisha nyota wake, lakini bado Simba ni tishio kwa timu pinzani kutokana na uzoefu wake katika michuano hiyo.
Nguvu ya Simba katika mashindano hayo inaonekana ipo eneo la ushambuliaji kwani mpaka sasa ina wachezaji watano, wanne wakiwa ni wapya ambao ni Mo Rashid, Salamba, Kaheza na Meddie Kagere aliyenyakuliwa kutoka Gor Mahia.
Kukosekana kwa nyota wake kadhaa kunaweza kuifanya Simba isiwe na makali sana hasa safu ya ushambuliaji kutokana na ukweli Emmanuel Okwi na Bocco wanapokosekana kikosini huwa kuna pengo linaloonekana dhahiri.
Pia, Simba inaweza kuyumba kidogo katika eneo la nyuma kwa kukosekana kwa kipa Aishi Manula na baadhi ya mabeki wa kazi walioibeba Simba katika VPL na michuano ya CAF.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE