Uongozi wa Simba umethibitisha kuachana na beki wake kisiki Juuko Murshid, raia wa Uganda.
Mapema leo Simba ilitambulisha usajili wa wachezaji watatu, Medie Kagere, Deo Munishi na Paschal Wawa ambaye imeelezwa amechukua nafasi ya Juuko.
Mkuu wa Idara ya Habari ya Klabu ya Simba Haji Manara amesema Juuko alikwenda nchini Afrika Kusini kufanya majaribio katika klabu ya Super Soort United na huenda akafanikiwa.
Lilikuwa ni suala la muda tu kutangazwa kuachwa kwa beki huyo wa Kimataifa wa Uganda ambaye inaelezwa hakuwa na mahusiano mazuri na baadhi ya viongozi wa Simba akituhumiwa kuwa mtovu wa nidhamu.
Kuwasili kwa Wawa na beki mwingine Mnigeria aliyekuwa akifanya majaribio katika klabu ya Simba, ilikuwa ni dalili ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kuwa mbioni kumtema Juuko.

ADVERTISE HERE