Uongozi wa Simba umesema umewapa mapumziko wachezaji wake waandamizi kutoshiriki michuano ya Kombe la Kagame inayoanza kutimua vumbi jijini Dar es salaam kesho.
Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo Haji Manara amewaambia waandishi wa habari leo kuwa katika michuano hii watawapa nafasi baadhi ya wachezaji wapya na wale ambao hawakupata nafasi ya kutosha kuitumikia Simba msimu uliomalizika.
Manara amesema baadhi ya wachezaji waandamizi wanastahili kupumzishwa baada ya kuichezea timu hiyo michezo mingi.
Miongoni mwa wachezaji ambao watakosa michuano hiyo ni pamoja na Aishi Manula, Shomari Kapombe, Nicolas Gyan, Jonas Mkude, Erasto Nyoni na Asante Kwasi.
Wengine ni Haruna Niyonzima, John Bocco na Emanuel Okwi.
Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Masudi Djuma ameunga mkono uamuzi wa wachezaji hao kupewa mapumziko.
"Tuna mashindano mengi mbele yetu. Ni vyema tukatumia michuano hii kuwapa nafasi wachezaji ambao hawakutumika sana."
"Lakini pia tuwape heshima baadhi ya wachezaji tunaoachana nao kwa kuwaaga kupitia michuano hii"
Simba itashuka dimbani Jumamosi, Juni 30 kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Dakadaha FC ya Somalia.

ADVERTISE HERE