Simba yawatambulisha Kagere, Wawa na Dida

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Jun 2018
Simba yawatambulisha Kagere, Wawa na Dida
Uongozi wa mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba umewatambulisha rasmi wachezaji wake wapya watatu Medie Kagere, Paschal Wawa na Deogratius Munishi 'Dida' waliosajiliwa kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Idara ya Habari ya Klabu ya Simba Haji Manara amesema wachezaji hao wamesajiliwa baada ya kuridhishwa na uwezo wao na watatumiwa na timu hiyo kwenye michuano mbalimbali watakayoshiriki msimu ujao.

Kagere aliyesajiliwa na Simba akitokea klabu ya Gor Mahia amekabidhiwa jezi namba 14 huku Pascal Wawa aliyesajiliwa akiwa mchezaji huru amekabidhiwa jezi namba 27.

Mlinda lango Deo Munishi 'Dida' yeye amekabidhiwa jezi namba 32.

Akizungumzia usajili wa wachezaji hao, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Masudi Djuma amesema anaamini uzoefu wao utaisaidia Simba msimu ujao.

"Hawa wote wana uzoefu wa soka la Kimataifa. Ili tuweze kuwa na timu imara tunahitaji wachezaji vijana na wakongwe kama hawa."
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
31m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’