Yanayojiri Urusi : Ujerumani yaondoshwa michuano ya kombe la dunia

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Jun 2018
Yanayojiri Urusi : Ujerumani yaondoshwa michuano ya kombe la dunia
Mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la dunia Ujerumani wameondoshwa kwenye michuano hiyo baada ya kulazwa mabao 2-0 na Korea Kusini.

Licha ya kumiliki mpira kwa muda mwingi, ubutu wa safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa mwaka 2014 umewaondosha mapema kwenye michuano hiyo.

Ujerumani imefunga mabao mawili pekee kwenye michuano hiyo, ikishinda mchezo mmoja dhidi ya Sweden na kupoteza michezo miwili.

Ujerumani imemaliza mkiani kundi F baada ya kipigo hicho na kuziacha Sweden na Mexico zikitinga hatua ya mtoano.

Sweden imemaliza kileleni kwenye kundi hilo baada ya kuifumua Mexico mabao 3-0.

Saa tatu usiku michezo miwili ya kundi E itapigwa sambamba ambapo Uswisi itachuana na Costa Rica huku Brazil ikiumana na Serbia
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
17h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
17h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
20h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’