Manara kuzungumzia usajili Alhamisi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Jun 2018
Manara kuzungumzia usajili Alhamisi
Mkuu wa Idara ya Habari ya Klabu ya Simba Haji Manara amesema siku ya Alhamisi, Juni 28 2018 atazungumza na Waandishi ya habari kutoa taarifa za michakato ya usajili inayoendelea.

Manara amesema wakati huu hawezi kuzungumzia jambo lolote kuhusu usajili hadi utakapokamilika kwa asilimia 100 hivyo amewataka wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba kuwa watulivu.

Leo Simba imekamilisha usajili wa Meddie Kagere kutoka klabu ya Gor Mahia ya Kenya huku ikiendelea kumjaribu beki mkongwe Paschal Wawa aliyewahi kuitumikia Azam FC.

Wakati huo huo kikosi cha Simba leo kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es salaam kujiandaa na michuano ya kombe la Kagame inayoanza mwishoni mwa wiki.

Simba imeendelea kufanya mazoezi bila ya wachezaji wake waandamizi ambao inadaiwa wamepewa mapumziko na hawatashiriki michuano hiyo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
16h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
19h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’