Klabu ya Simba imemalizana na mshambuliaji tegemeo wa Gor Mahia Meddie Kagere ambaye wakala wake amethibitisha amesaini mkataba wa miaka miwili.
Ingawa bado uongozi wa Simba haujatoa taarifa rasmi kuhusu kukamilika kwa usajili wa Kagere aliye nchini tangu jana, picha inayomuonyesha mchezaji huyo akisaini mkataba mbele ya Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah 'Try Again' akishuhudiwa na wakala wake imesambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Kagere anakuwa mshambuliaji wa nne kusajiliwa na Simba baada ya mabingwa hao wa Tanzania Bara pia kukamilisha usajili wa washambuliaji watatu wa ndani, Adam Salamba, Mohammed Rashid na Marcel Kaheza

ADVERTISE HERE