Patrick Gakumba ndiye wakala wa mchezaji kinara wa mabao katika klabu ya Gor Mahia Meddy Kagere ambaye yuko nchini tayari kujiunga na mabingwa soka Tanzania Bara, Simba.
Akihojiwa na EFM, Gakumba amesema wamekuja nchini baada ya kupokea ofa ya klabu ya Simba kutaka kumsajili Kagere ambaye mkataba wake wa kuitumikia Gor Mahia uko ukingoni.
Gakumba amesema mazungumzo yao yanakwenda vizuri lakini taarifa zaidi zitatolewa punde kila kitu kitakapokuwa kimekamilishwa.
Kagere ndiye kinara wa mabao kwenye kikosi cha Gor Mahia.
Hivi karibuni aliibuka kuwa mfungaji bora wa michuano ya SportPesa Super Cup kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuifungia timu hiyo mabao manne.
Taarifa ya Kagere kuwa nchini kumalizana na Simba zimewashitua mashabiki wa Gor Mahia ambao wameujia juu uongozi wa timu yao wakitaka wapatiwe maelezo kwa nini mchezaji huyo hakusaini mkataba mpya kwa wakati mpaka anaondoka akiwa mchezaji huru.
Mbali na Kagere, Simba inaweza kumsajili kiungo, roho wa Gor Mahia Francis Kahata ambaye pia mkataba wake wa kuitumikia timu hiyo unaelekea ukingoni.
Kutua kwa Kagere Simba ni dhahiri kutaongeza uimara wa kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania kitachoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa baadae mwaka huu.

ADVERTISE HERE