Yanayojiri Urusi : Nigeria yasaka tiketi mbele ya Argentina iliyojeruhiwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Jun 2018
Yanayojiri Urusi : Nigeria yasaka tiketi mbele ya Argentina iliyojeruhiwa
Nigeria ina nafasi ya kupenya hatua ya mtoano ya michuano ya kombe la dunia kama itashinda au pengine hata kupata sare katika mchezo wake wa leo wa kundi D dhidi ya Argentina.

Mchezo huo utakaopigwa saa tatu usiku unatarajiwa kuwa na upinzani wa kipekee kwa kuwa hata Argentina inaweza kutinga hatua hiyo kama itaibuka na ushindi.

Ushindi wa mabao 2-0 iliyopata Nigeria dhidi ya Iceland kwenye mchezo uliopita umefufua matumaini ya timu hiyo kutinga hatua ya mtoano.

Lakini itabidi ifanye kazi ya ziada dhidi ya Argentina 'iliyojeruhiwa' kwa kubamizwa mabao 3-0 na Croatia kwenye mchezo uliopita.

Argentina itakuwa inasaka ushindi wake wa kwanza kwenye michuano hiyo, ushindi ambao unaweza ukatosha kuwavusha hatua ya mtoano.

Iceland yenye alama moja sawa na Argentina itakuwa ikichuana na Croatia ambayo tayari imefuzu.

Wakati sare inaweza kuivusha Nigeria, Argentina na Iceland lazima zishinde michezo yao kabla ya masharti mengine kutumika kubaini timu itakayofuzu.

Mapema saa tisa kutakuwa na michezo miwili ya kundi C ambapo Autralia itachuana na Peru huku Ufaransa ambayo tayari imefuzu ikichuana na Denmark.

Denmark inahitaji sare tu kuungana na Ufaransa hatua inayofuata wakati Australia ni lazima ishinde huku ikiomba Denmark ifungwe na Ufaransa.

Jana Hispania na Ureno zilitinga hatua ya mtoano licha ya kulazimishwa sare kwenye michezo yao ya mwisho hatua ya makundi.

Hispania ililazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Morocco huku Ureno ikilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Irani katika michezo ambayo Morocco na Irani zingeweza kushinda kirahisi.

Hispania sasa itachuana na Urusi kwenye hatua ya 16 bora baada ya kumaliza ya kwanza kundi B wakati Ureno itakabiliana na uruguay kwenye hatua hiyo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’