Klabu ya Simba imethibitisha kuwa beki wa zamani wa Azam FC Paschal Wawa atakuwa kwenye kikosi cha Simba kitakachoshiriki michuano ya kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba Said Tully amethibitisha kuwa timu hiyo kwenye mazungumzo ya kumsajili beki huyo mkongwe na yanakwenda vizuri.
"Wawa ataichezea Simba kwenye michuano ya kombe la Kagame na hatma yake itatangazwa baada ya kumalizika kwa michuano hiyo," amesema Tully.
Wawa alianza kuonekana akifanya mazoezi kwenye kikosi cha Simba jana ikiwa ni siku moja tu tangu awasili kutoka kwao Ivory Coast.
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 yuko huru baada ya Mkataba wake wa kuitumikia El Mareikh kumalizika.

ADVERTISE HERE