Shirikisho la soka nchini (TFF) leo limetoa mafunzo ya matumizi ya mfumo mpya wa usajili (TFF FIFA CONNECT) kwa vilabu vya ligi Kuu.
Afisa wa Usajili wa TFF Baraka Kizuguto amesema mfumo huo unalenga kurahisisha mchakato wa usajili pamoja na kuondoa udanganyifu.
Kizuguto amewataka Mameneja wa usajili wa vilabu kuhakikisha wanajaza taarifa sahihi za wachezaji kama inavyoelekezwa.
Kizuguto amesema baada ya zoezi la usajili kukamilika kwa timu za ligi kuu, daraja la kwanza na la pili taarifa za wachezaji zitakuwa mahali pamoja hivyo kurahisisha mchakato wachezaji wanapohama kutoka timu moja kwenda nyingine.
Zoezi la utolewaji wa mafunzo litaendelea kesho kwa timu za daraja la kwanza na kukamilishwa keshokutwa kwa timu za daraja la pili.

ADVERTISE HERE