Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema timu hiyo ilijipanga ndio maana imezifunika klabu zote zilizoshiriki Ligi Kuu msimu ulioisha kwa kunyakua tuzo nyingi zilizotolewa jana Jumamosi usiku kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Manara amesema Simba imejipanga vyema kwa ajili ya msimu ujao ili kuweza kufanya vizuri zaidi licha ya kuongezeka timu na kufikia 20.
Amesema suala la kuongezeka timu halimpi tatizo bali miundombinu kwa ujumla kwani itazilazimu timu kusafiri umbali mrefu zaidi.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara waliibuka na kitita cha Sh 96 milioni baada ya kufanikiwa kutwaa taji hilo.
Katika halfa ya utoaji wa tuzo hizo, Simba ilipenyeza wachezaji watano kwenye kikosi bora cha cha Ligi Kuu msimu ulioisha.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE