Yanayojiri Urusi : Ujerumani yafufua matumaini ya kutinga mtoano

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Jun 2018
Yanayojiri Urusi : Ujerumani yafufua matumaini ya kutinga mtoano
Ujerumani ilibidi ifanye kazi ya ziada kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sweden na kufufua matumaini ya kutinga hatua ya mtoano.

Licha ya kutawala mchezo kwa zaidi ya asilimia 70, Ujerumani ilijikuta nyuma kwenye dakika 30 baada ya Sweden kufunga bao kupitia shambulizi la kushitukiza, Ola Toivonen akiuweka mpira kambani.

Marco Reus aliwarudisha Ujerumani, mabingwa watetezi mchezoni kwa bao safi kwenye dakika ya 48 kabla Toni Kroos hajafunga bao la ushindi kwenye dakika za majeruhi.

Ujerumani ilimaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji 10 baada mlinzi Jarome Boateng kutolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.

Mapema Ubelgiji ilitinga hatua ya mtoano baada ya kuilaza Tunisia mabao 5-2, Romelu Lukaku na Eden Hazard wakifunga mabao mawili kila mmoja.

Lukaku amefikisha mabao manne kwenye michuano hiyo akimfikia mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo.

Tunisia imekuwa timu ya tatu kutoka Afrika kuyaaga mashindano hayo. Misri na Morocco zilikuwa za kwanza kuondolewa mashindanoni.

Nayo Mexico imetinga hatua ya mtoano baada ya kuilaza Korea Kusini mabao 2-1.

Kesho wawakilishi wa Afrika Senegal watashuka dimbani kwa mara ya pili katika michuano hiyo wakiikabili Japani mchezo utakaopigwa saa 12 jioni.

Senegal inaweza kutinga hatua ya mtoano kama itaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Mapema kabla ya mchezo huo, saa tisa Alasiri Uingereza itapepetana na Panama wakati mchezo wa saa tatu usiku itakuwa kati ya Poland dhidi ya Colombia
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
31m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’