Yanayojiri Urusi : Nigeria yawatoa kimasomaso Waafrika, yaichapa Iceland 2-0

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Jun 2018
Yanayojiri Urusi : Nigeria yawatoa kimasomaso Waafrika, yaichapa Iceland 2-0
Nigeria imewatoa 'kimasomaso' Waafrika baada ya kuilaza Iceland mabao 2-0 katika mchezo wa kombe la Dunia, kundi D.

Baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza kwa mabao 2-0 dhidi ya Croatia, Nigeria ilihitaji kushinda mchezo wa leo ili kufufua matumaini ya kusonga mbele hatua ya 16 bora.

Nigeria ilifunga mabao yake yote mawili kwenye kipindi cha pili kupitia kwa winga mwenye kasi Ahmed Mussa.

Iceland ilipoteza mkwaju wa penati wakati mchezo huo ukielekea mwishoni.

Matokeo hayo yanaifanya Nigeria ipande mpaka nafasi ya pili kundi D baada ya kufikisha alama tatu na kuziacha Iceland na Argentina zikishika nafasi ya tatu na nne zikiwa na alama moja moja.

Kimahesabu, Nigeria huenda ikahitaji sare tu kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Argentina ili iweze kuungana na Croatia kutinga hatua ya mtoano.

Mapema Brazil iliilaza Costa Rica mabao 2-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya 16 bora.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’