TFF yaja na mfumo mpya wa usajili

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Jun 2018
TFF yaja na mfumo mpya wa usajili
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limefungua rasmi dirisha la usajili kwa msimu wa 2018/2019 ambapo usajili wa awamu hii utakuwa ni usajili wa tofauti utakaotumia mfumo mpya ujulikanao kwa jina la TFF FIFA CONECT.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Habari cha TFF, Clifford Ndimbo amesema kabla ya kuanza rasmi kutumika kwa mfumo huo, klabu zinazoshiriki Ligi Kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili zitapewa semina jinsi ya matumizi ya mfumo huo.

"Semina hii itakuwa ya siku tatu ambapo tutaanza na klabu za ligi kuu Jumatatu ijayo Juni 25, Jumanne tutakuwa na ligi daraja la kwanza na jumatano tutamalizia na Ligi daraja la pili.

"Tunaziomba klabu zote zizingatie muda wa kuja kupewa mafunzo haya ili isije kuleta shida baadaye," amesema Ndimbo

Aidha, amesema baada ya kumalizika kwa usajili huo kutakuwa na wiki moja ya mapingamizi na klabu mbalimbali vitawasilisha mapingamizi katika kamati maalumu itakayosimamia suala la usajili.

Dirisha la usajili msimu wa 2018/2019 lilifunguliwa Juni 15, na litafungwa Julai 26, mwaka huu ambapo Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji itakuwa na wiki moja ya kupitia mapingamizi yatakayowasilishwa na klabu husika kama yatakuwepo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’