Yanayojiri Urusi : Argentina hatarini, Nigeria kibaruani leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Jun 2018
Yanayojiri Urusi : Argentina hatarini, Nigeria kibaruani leo
Argentina imejiweka katika mazingira magumu ya kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Urusi baada ya kulazwa mabao 3-0 na Croatia jana.

Licha ya uwepo wa kinara Lionel Messi na kikosi kilichojaa nyota wengi, hali ilikuwa tete kwa Argentina mbele na Croatia iliyokuwa haikamatiki.

Kichapo hicho kinaiweka Argentina hatarini kushindwa kufuzu raundi ya pili ya michuano hiyo kwani watalazimika kushinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Nigeria huku pia wakiomba Iceland ishindwe kuibuka na ushindi mbele ya Nigeria leo.

Nayo Nigeria inahitaji kushinda mchezo wake wa leo dhidi ya Iceland utakaopigwa saa 12 jioni ili kufufua matumaini ya kutinga hatua ya 16 bora.

Iceland ina alama moja sawa na Argentina wakati Nigeria itakuwa inasaka matokeo yake ya kwanza kwenye michuano hiyo baada ya kulazwa mabao 2-0 na Croatia kwenye mchezo wa kwanza.

Croatia imeungana na Uruguay, Urusi na Ufaransa kuwa timu za kwanza kutinga hatua ya 16 bora.

Ushindi wa bao 1-0 iliyopata Ufaransa dhidi ya Peru uliifanya timu hiyo ifikishe alama sita ikifuatiwa na Denmark yenye alama nne baada ya jana kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Australia.

Ukiacha mchezo wa Nigeria dhidi ya Iceland utakaopigwa saa 12, leo kutakuwa na michezo mingine miwili ambapo mchezo wa mapema saa tisa utakuwa ni Brazil dhidi ya Costa Rica wakati Serbia itaikabili Uswisi saa tatu usiku.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’