Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Djuma, baada ya kuifuatilia Yanga kupitia mikanda ya video amesema ni rahisi kwa Simba kupata ushindi dhidi yao.
“Nimewaona Yanga ni rahisi kuwazuia kwani wachezaji wao wengi hawatumii nguvu wanatumia akili kuliko nguvu, kwa hiyo na sisi tumewapa wachezaji wetu mazoezi ya kimbinu zaidi ili kuwazidi wapinzan," amefunguka Djuma
“Kutokana na ukubwa wa mechi hii kila mchezaji atakuwa fiti ila yule mwenye utimamu wa kimwili ndio atakuwa msaada mkubwa kwa timu yake kwahiyo tuna uhakika wa asilimia zote kuwa wachezaji wetu wana utimamu huo ambao ndio siri kubwa ya ushindi kwetu.
“Mechi yoyote ya dabi huwa inatawaliwa na mambo mengi, lakini mambo yote ya msingi ya ndani ya uwanja tumeshayamaliza kama benchi la ufundi na jukumu limebaki kwa wachezaji kufanya kazi yao.
“Ila pia tunaomba sapoti ya mashabiki kwa wingi kwenye mechi hii kwani shabiki ni mchezaji wa kumi na mbili.â€
Kocha huyo mpya kikosini humo, pia amewataja wachezaji wa Yanga kwa kusema: “Ajibu (Ibrahim) si mchezaji wa kumuachia acheze kwa nafasi kwani anaweza kuwa na madhara kwetu, kwa nilivyomuona ni miongoni mwa wachezaji wa kuwachunga, ni mzuri wa kupiga faulo katika maeneo ya karibu.
“Chirwa (Obrey) ana uwezo wa kukimbia na ana nguvu ya kushindana na mabeki, tumejipanga kukabiliana naye, lakini pia sisi tumeshaweka sawa mipango yetu ya ushindi.â€

ADVERTISE HERE