Senegal imekuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kupata ushindi kwenye michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Urusi baada ya kuilaza Poland mabao 2-1.
Bao la kujifunga la Cionek kwenye dakika ya 37 na bao lililofungwa na Niang kwenye dakika ya 60 baada ya uzembe uliofanywa na Grzegorz Krychowiak, yalitosha kuipa ushindi muhimu Senegal.
Krychowiak alifuta makosa yake kwa kuifungia Poland bao la kufutia machozi kwenye dakika ya 86.
Ushindi huo umepokewa kwa furaha na Waafrika hasa ikizingatiwa Senegal imekuwa timu ya kwanza kupata ushindi miongoni mwa timu zinazowakilisha Afrika.
Senegal sasa inaongoza kundi G ikiwa na alama tatu sawa na Japan ambayo pia ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Colombia kwenye mchezo wa mapema

ADVERTISE HERE