Yanayojiri Urusi : Bundi aendelea kuzitembelea timu za Afrika

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Jun 2018
Yanayojiri Urusi : Bundi aendelea kuzitembelea timu za Afrika
Jana Tunisia ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Uingereza ikiendeleza uteja wa timu za Afrika kwenye michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko Urusi.

Uingereza ilitangulia kufunga mapema tu kwa bao la mshambuliaji Harry Kane aliyefunga kwenye dakika ya 10. Sassi aliisawazishia Tunisia bao hilo kupitia mkwaju wa penati kwenye dakika ya 35.

Licha ya kujilinda kwa muda mwingi, Tunisia iliruhusu bao la pili kwenye dakika za majeruhi, Kane akifunga bao hilo likiwa la pili kwake na kwa Uingereza.

Tunisia ilipiga shuti moja pekee lililolenga lango la Uingereza katika muda wote wa dakika 90 za mchezo.

Hakuna timu ya Afrika ambayo mpaka sasa imeshinda huko Urusi baada ya Misri, Morocco na Nigeria zote kuwa zimefungwa kwenye michezo yao ya awali.

Michezo mingine iliyopigwa jana iliishuhudia Ubelgiji ikiilaza Panama mabao 3-0, Romelu Lukaku akifunga mabao mawili, wakati Sweden ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Korea Kusini kwenye mchezo wa mapema

Leo kutakuwa na michezo mitatu, ambapo wawakilishi wengine wa Afrika, Senegal watakamilisha mzunguuko wa kwanza wa michuano hiyo kwa kumenyana na Poland saa 12 jioni.

Mchezo wa mapema saa tisa Alasiri ni kati ya Colombia dhidi ya Japan.

Saa tatu usiku michuano hiyo itaingia kwenye mzunguuko wa pili kwa wawakilishi wa Afrika kutoka kundi A Misri kucheza na Urusi.

Huenda mshambuliaji tegemeo wa Misri Mohammed Salah akacheza mchezo huo baada ya kukosa mchezo wa kwanza.

Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Uruguay, Misri inahitaji kushinda mchezo huo ili kufufua matumaini ya kutinga hatua ya mtoano.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’