Wiki hii kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba kinaanza kujiwinda tayari kwa michuano ya kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Juni 29 katika viwanja vya Taifa na Azam Complex, Chamazi.
Wachezaji wa Simba walipewa mapumziko ya wiki nzima baada ua kurejea kutoka nchini Kenya kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup.
Hata hivyo Simba huenda ikawapumzisha baadhi ya nyota wake kushiriki michuano hiyo baada ya kutumika kwa muda mrefu.
Simba itashuka uwanja wa Taifa Juni 30 kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Dakadaha ya Somalia.
Simba iko kundi C pamoja na St George, Dakadaha na Al Hilal (Sudan) baada ya Yanga kujiondoa kwenye michuano hiyo.

ADVERTISE HERE