Mshambuliaji wa Simba, John Bocco, amesema timu hiyo itafanya vizuri zaidi msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.
Bocco, ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Simba msimu uliomaliika, amesema usajili uliofanywa na timu hiyo utaongeza ushindani wa namba kwenye timu na hivyo kuifanya Simba kuendelea kuwa moto mbele ya wapinzani wao.
Tayari Simba imewasajili washambuliaji watatu waliofanya vizuri msimu uliopita ambao ni Adam Salamba kutoka Lipuli, Marcel Kaheza (Majimaji) pamoja na Mohamed Rashid(Prisons).
"Mimi nafikiri kikosi kitaimarika zaidi, ushindani wa namba utaongezeka, lakini pia kila mmoja anataka kuona tunafanya vizuri..., naamini tutafanya vizuri zaidi ya msimu huu ulioisha," alisema Bocco.
Nyota huyo alisema kwa kuanzia wanataka kufanya vizuri kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame.
Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Juni 28, mwaka huu jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa na Azam Complex.
"Tunajipanga kwa ajili ya Kagame..., michuano hii itatuweka sawa kuelekea Ligi Kuu msimu ujao," alisema Bocco.

ADVERTISE HERE