Kuwapo kwa mvua ni dalili mojawapo ya mashabiki wa Simba kuamini timu yao itaibuka na ushindi pale wanapokutana na watani zao Yanga, Kocha Mkuu wa wekundu wa msimbazi, Joseph Omog, amesema kuwa kikosi chake kinasubiri muda wa mchezo ufike huku akieleza wapinzani wao wataponzwa na wasiwasi.
Yanga ambao ni wenyeji wanatarajiwa kuikaribisha Simba katika mchezo huo wa kwanza msimu huu ambao utafanyika kesho kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Omog, anasema kuwa mbali na mazoezi ya uwanjani, amewaandaa wachezaji wake wasiwe na hofu au wasiwasi wa aina yoyote wakati watakaposhuka uwanjani kucheza na mabingwa hao watetezi.
Omog amesema wachezaji ambao wana wasiwasi, ni vigumu kuipa timu matokeo mazuri na anaamini hilo halitakuwapo kwenye kikosi chake.
"Wasiwasi inaweza kuigharimu timu, kwa upande wangu ninawakumbusha wachezaji kuiona mechi hiyo kama mechi nyingine ambazo tumecheza na tutacheza baada ya Jumamosi, kuwa watulivu na kuwa na nidhamu ya uwanjani, sijui kwa upande wa wapinzani wetu," alisema Omog.
Aliongeza kuwa anaamini timu itakayoshinda katika mechi hiyo ya kesho, itakuwa imejiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi ambao utakuwa umebakisha michezo saba ili mzunguko wa kwanza umalizike.
"Tuna nguvu mpya kwenye benchi letu la ufundi, naamini pia mambo mapya yataonekana uwanjani kupitia msaidizi wangu, tunasaidiana vyema kwa sababu lengo letu ni moja la kupata pointi tatu," alisema kocha huyo ambaye aliwahi pia kuifundisha Azam FC.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa kikosi chao jana asubuhi kiliendelea kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Amaan.
Simba tayari imerejea Dar.
Simba na Yanga kila moja ina pointi 15 lakini Wekundu wa Msimbazi wanaongoza kutokana na kuwa na mabao mengi ya kufunga wakati pia Mtibwa Sugar inayoshika nafasi ya tatu inapointi sawa na wakongwe hao.

ADVERTISE HERE