Wakati wa maandalizi kuelekea michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko Urusi, Ujerumani haikuwa na mwenenendo mzuri hivyo kuwapa hofu wengi juu ya uwezo wao ya kutetea taji hilo walilotwaa nchini Brazil mwaka 2014.
Hofu ya wengi imedhihirika baada ya hapo jana Ujerumani kuanza vibaya michuano hiyo kwa kuchapwa bao 1-0 na Mexico.
Bao la kinda Lozano alilofunga kwenye dakika ya 35 lilidumu hadi filimbi ya kumaliza mchezo huo ilipopulizwa licha ya Ujerumani kulisakana lango la Mexico kwenye dakika za majeruhi.

Mexico ingeweza kushinda mchezo huo kwa mabao mengi zaidi kama washambuliaji wake wangekuwa makini kwani kupitia mashambulizi yao ya kushitukiza, walitengeneza nafasi nyingi.
Mchezo wa mapema uliishuhudia Serbia ikiilaza Costa Rica kwa bao 1-0, bao lililowekwa kambani na Alexander Kolarov.
Mchezo wa mwisho siku ya jana uliishuhudia Brazil ikilazimishwa sare ya bao 1-1 na Uswisi.
Philippe Coutinho aliitanguliza Brazil kwenye dakika ya 20 kwa shuti kali nje ya 18 lakini Uswisi ikasawazisha kwenye dakika ya 50 kupitia mpira wa kichwa wa Zuber.
Hata hivyo bao hilo lilipingwa vikali na wachezaji wa Brazil bila mafanikio kwani Zuber alionekana akimsukuma mlinzi Miranda kabla ya kuujaza mpira wa kona kimiani kwa kichwa.
Brazil ilimaliza mchezo huo kufanya mashambulizi mfululizo langoni kwa Uswisi lakini jitihada zao hazikuzaa matunda.
Michuano ya kombe la dunia inaendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa.
Mchezo wa mapema saa tisa ni wa kundi F kati ya Sweden dhidi ya Korea Kusini ukifuatiwa na mchezo wa kundi G kati ya Ubelgiji dhidi ya Panama saa 12 jion.
Tunisia, timu nyingine kutoka Afrika itashuka dimbani saa tatu usiku kuikabili Uingereza katika mchezo mwingine wa kundi G.

ADVERTISE HERE