Yanayojiri Urusi : Timu za Afrika majanga!

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Jun 2018
Yanayojiri Urusi : Timu za Afrika majanga!
Misri ililazwa bao 1-0 na Uruguay kwenye mchezo wa mapema wa kombe la dunia uliopigwa jana huko Urusi.

Vijana wa Misri wakicheza bila kinara wao Mo Salah ambaye aliachwa nje licha awali kocha wa timu hiyo kubainisha angecheza, walishindwa mapambano kwenye dakika za majeruhi kwa Uruguay kufunga bao pekee katika dakika ya 89 likifungwa na Gimenez.

Majanga kama hayo yakawakumba Morocco ambao walichapwa bao 1-0 na Irani katika mchezo ambao itabidi wajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuibuka na ushindi.

Bao la kujifunga la Bouhaddouz kwenye dakika za lala salama, liliihakikishia Irani ushindi wa kushitukiza.

Kipigo hicho kimewaweka Morocco kwenye wakati mgumu wa kufuzu hatua ya mtoano kwani watahitaji kuibuka na ushindi dhidi ya Uhispania na Ureno.

Leo kutakuwa na michezo minne ya kundi C na D ambapo saa nne usiku waafrika wengine Nigeria watachuana na Croatia.

Mchezo wa mapema, saa saba Ufaransa itachuana na Australia kisha kufuatiwa na mchezo kati ya Argentina dhidi ya Iceland saa kumi.

Peru na Denmark zitaumana saa moja jioni.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’