Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limeialika klabu ya Vipers SC kutoka nchini Uganda kuchukua nafasi ya Yanga iliyojitoa kwenye michuano ya kombe la Kagame inayoanza Juni 28 jijini Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye amesema wameridhia maombi ya Yanga kujitoa kwenye mashindano hayo na tayari timu hiyo kutoka Uganda imeshapelekewa mwaliko rasmi.
Wiki iliyopita Yanga ilijiondoa kwenye mashindano hayo ikieleza kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa kikosi chao.
Hata baada ya kupewa saa 48 kufikiria upya uamuzi huo, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisisitiza uamuzi wa kujitoa uko palepale.
Vipers FC inaungana na timu nyingine za kundi C ambazo ni Simba, Dakadaha ya Somalia na St. George ya Ethiopia.

ADVERTISE HERE