Mavugo afunguka hatma yake Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Jun 2018
Mavugo afunguka hatma yake Simba
Mshambuliaji wa Simba raia wa Burundi Laudirt Mavugo amesema mkataba wake unamalizika Julai 05 mwaka huu na bado hajasaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Mavugo ambaye yuko Burundi kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa amesema yuko tayari kubaki katika klabu ya Simba kama atahitajika.

Mavugo amebainisha kwamba Simba walimpa ofa ya kuongeza mkataba wake kwa mwaka mmoja lakini amekataa akitaka apewe mkataba wa angalau miaka miwili.

Mshambuliaji huyo aliyetua kwa mbwembwe nchini misimu miwili iliyopita amesema tayari ana ofa nne mezani kutoka Yanga, Singida United, Gor Mahia na AFC Leopards.

Mavugo ana nafasi finyu ya kubaki Simba hasa baada ya klabu hiyo kukamilisha usajili wa washambuliaji watatu, Adam Salamba, Mohammed Rashid na Marcel Kaheza.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
14h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
17h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’