Mwinyi afuta kauli ya 'Tanzania kwenye soka ni kama kichwa cha Mwendawazimu'

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
12 Jun 2018
Mwinyi afuta kauli ya 'Tanzania kwenye soka ni kama kichwa cha Mwendawazimu'
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameamua kufuta kauli yake aliyoisema mwaka 1993, kwenye Uwanja wa Uhuru kwamba Tanzania katika soka ni kichwa cha mwendawazimu.

Rais Mwinyi alitoa kauli ya hiyo baada ya kuishudia Simba ikichapwa mabao 2-0 katika fainali ya Kombe la CAF (saa Kombe la Shirikisho Afrika) na Stella Club d'Adjame ya Ivory Coast.

Miaka 25, baadaye Rais Mwinyi ameifuta kauli hiyo alipokuwa katika ugawaji tuzo za Simba ‘Mo Awards’, ambapo alionekana kama amefurahia tukio hilo na kuamua futa kauli yake hiyo.

“Ndugu zangu kuanzia leo nafuta ile kauli yangu, najua mnaikumbuka kwahiyo naiondoa kabisa siku ya leo,” alisema maneno hayo kisha akaomba kuondoka ukumbini hapo baada ya kutoa tuzo ya Heshima aliyochukua Seleman Matola.

Wachezaji waliofanikiwa kuchukua tuzo Aish Manula (Kipa Bora), Erasto Nyoni (Beki bora wa mwaka), Shiza Kichuya (Kiungo Bora), Emmanuel Okwi (Mshambuliaji Bora wa Mwaka), Zainab Rashid Pazi (Mchezaji Bora wa kike), Rashid Juma ( Mchezaji Bora Chipukizi), Goli bora la mwaka (John Bocco), Masoud Djuma, Piere Lechantre, Abbas Seleman na Mohammed Habib (Tuzo ya benchi la ufundi), Saleh Kambi (Shabiki Bora), Hamis Mwinjuma ‘Mwana Fa’ (Mhamasishaji wa mitandaoni).

Wengine ni Haji Manara (Mhamasishaji), Seleman Matola (Tuzo ya Heshima), Ubungo Terminal (Tuzo ya Tawi Bora), Salim Abdallah (Kiongozi bora wa mwaka), John Bocco (Mchezaji Bora wa Mwaka)

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
29m ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →