Simba kusajili washambuliaji wa Kimataifa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Jun 2018
Simba kusajili washambuliaji wa Kimataifa
Michuano ya SportPesa Super Cup iliyomaliza kwa Gor Mahia kuhifadhi taji hilo kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuifunga Simba mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali, imeugutusha uongozi wa mabingwa hao wa Tanzania Bara na wamepanga kusajili washambuliaji wa Kimataifa.

Simba itashiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika inayotarajiwa kuanza mwezi Disemba mwaka huu, inahitaji kuimarisha safu yake ya ushambuliaji licha ya usajili wa washambuliaji watatu uliofanyika msimu huu.

Marcel Kaheza, Adam Salamba na Mohammed Rashid waliosajiliwa na Simba hivi karibuni, walijumuishwa kwenye kikosi cha Simba kilichoshiriki michuano ya SportPesa nchini Kenya lakini walishindwa kuonyesha makali yao.

Ni Adam Salamba pekee ambaye kidogo aliongeza uhai kwenye safu ya ushambuliaji ya Simba baada ya kusafirishwa kuongeza nguvu kuanzia hatua ya nusu fainali.

Ingawa bado ni mapema, tayari kumekuwa na ukosoaji kwa usajili wa washambuliaji hao baadhi ya wadau wakikosoa usajili huo kuwa ulifanywa kwa pupa na wa kuwafurahisha mashabiki bila ya kuangalia mahitaji ya timu hasa ya michuano ya Kimataifa.

Kwani licha ya uwepo wa washambuliaji hao, Simba bado inaonekana itakuwa na wakati mgumu kwenye michuano hiyo kama itawakosa washambuliaji wake tegemeo nahodha John Bocco na Emanuel Okwi.

Bocco na Okwi hawekuwemo kwenye kikosi kilichoshiriki mashindano ya SportPesa ambayo yalimalizika bila ya Simba kufunga bao zaidi ya mikwaju ya penati.

Kwa sasa safu ya ushambuliaji ya Simba ina wachezaji watano baada ya usajili wa washambuliaji hao watatu.

Washambuliaji Laudirt Mavugo na Juma Liuzio wameachwa rasmi na mabingwa hao wa Tanzania Bara.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
44m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’