Mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji leo atatoa tuzo kwa wachezaji, viongozi na mashabiki waliochangia kwa nafasi zao kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu.
Tuzo hizo zitatolewa leo Hyatt Rgency - Kilimanjaro Hotel.
Hafla itaanza saa 12 kamili jioni na itarushwa mbashara nha kituo cha runinga cha Azam kupitia chaneli ya Azam Sport 2.
Tuzo hizo zitakuwa na vipengele 16, ambavyo ni Mchezaji Bora wa Mwaka, Goli Bora la Mwaka, Golikipa Bora wa Mwaka na Beki Bora wa Mwaka.
Pia Kiungo Bora wa Mwaka, Mshambuliaji Bora wa Mwaka, Shabiki Bora wa Mwaka na Tuzo ya Heshima.
Tuzo zingine ni Mchezaji Bora Mwanamke wa Mwaka, Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka, Tuzo ya Benchi la Ufundi, Kiongozi Bora wa Mwaka, Tuzo ya Wasimamizi wa Mchakato wa Mabadiliko, Mhamasishaji Bora wa Mwaka katika Mitandao ya Kijamii, Mhamasishaji Bora wa Mwaka na Tawi Bora la Mwaka.
Washindi wa tuzo hizo wamepatikana kwa kupigiwa kura na wadau kupitia mitandao rasmi ya kijamii ya klabu ya Simba na tovuti maalumu ya tuzo hizo.

ADVERTISE HERE