Lechantre akaribishwa tuzo za Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Jun 2018
Lechantre akaribishwa tuzo za Simba
Jioni ya leo Jumatatu, Juni 11 2018 Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji ameandaa hafla ya kugawa tuzo kwa wadau wa klabu ya Simba ambao mchango wao umefanikisha kuibuka mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu.

Tuzo hizo zitatolewa kwa viongozi, wachezaji na mashabiki ambapo washindi wamepigiwa kura na wadau.

Miongoni mwa wanaotarajia kuhudhuria tuzo hizo ni Kocha Mkuu wa klabu hiyo Pierre Lechantre ambaye aliikacha timu Nakuru, Kenya wakati inashiriki michuano ya SportPesa Super Cup iliyomalizika jana.

Lechantre aliiacha Simba mikononi mwa kocha msaidizi Masudi Djuma ikiwa kwenye hatua ya nusu fainali sababu ikielezwa kuwa na mgogoro wa viongozi juu ya masuala ya mkataba.

Kocha huyo anatarajiwa kupokea tuzo kwa niaba ya benchi lake la ufundi na huenda akaondoka baada ya hafla hiyo.

Bado uongozi wa Simba haujatoa taarifa rasmi juu ya hatma ya Lechantre ambaye mkataba wake unamalizika Juni 18, 2018.

Lakini taarifa za ndani zinabainisha kuwa Simba tayari imeamua kuachana na Lechantre kutokana na mahitaji yake makubwa ya mshahara na 'bonus'.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’