Kikosi cha Simba kimerejea nchini usiku wa kuamkia leo kutoka Kenya kushiriki mashindano ya SportPesa Super Cup.
Simba ilitinga fainali ya michuano hiyo ambapo ilipoteza mchezo wa fainali kwa kufungwa mabao 2-0 na Gor Mahia, iliyotwaa taji hilo kwa msimu wa pili mfululizo.
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema wachezaji watapewa mapumziko ya siku kadhaa kabla ya kuanza maandalizi ya michuano ya kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Juni 28 2018 jijini Dar es salaam.
Licha ya Yanga kujitoa kwenye mashindano ya Kagame, uongozi wa Simba umesema hauna mpango wa kujitoa, watashiriki kikamilifu.
Wachezaji wa Simba wamewahi kurejea ili kuwahi tuzo za Mo Simba Awards zinazotolewa leo Kilimanjaro Hotel kuanzia saa 12 kamili jioni.

ADVERTISE HERE